... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uhakika wa Wokovu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 5:24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.

Listen to the radio broadcast of

Uhakika wa Wokovu


Download audio file

Watu wengi sana wamechanganikiwa kuhusu kigezo kikubwa, kigezo pekee cha kupata uzima wa milele.  Wachache wanasema hivi, Mimi sijawa mtu mbaya sana, nitakuwa salama tu.  Wengine wanajiuliza, Je!  Mwishowe nitakuwa nimestahili?

Sasa niambie, je!  Umestahili vya kutosha?  Mimi sistahili wala sitastahili kamwe.  Angalia, mimi si mtu mbaya.  Nimeishi maisha sawa mpaka sasa na hata wewe unaweza kuniambia hivyo.  Lakini hakuna aliyeishi maisha mazuri ya kumridhisha Mungu.  Sisi sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wake, yaani kiwango cha kuwa mkamilifu asilimia mia.

Ndiyo maana Yesu alikuja kwa ajili yako na kwa ajili yangu; ili afe pale Msalabani alipe zile gharama za dhambi zetu haki ya Mungu inayodai; akafufuka tena ili atupe karama ya maisha mapya hapa duniani na uzima wa milele mbele zake, milele daima.

Je!  Mtu atayashikiliaje?  Kwa kujitahidi zaidi?  Kwa kujaribu kuwa mtu mwema?  Sikiliza alivyoeleza Yesu mwenyewe:

Yohana 5:24  Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.

Mtu anashikilia uzima wa milele kwa kumwamini Yesu tu.  Kwa imani ndani ya bei ya ukombozi aliyolipa pale Msalabani, kwa kuamini kwamba hatia yetu na hukumu tunayostahili kupokea ilimwangukia yeye, hapo ndipo mtu atakuwa amepata uzima wa milele.

Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele … amepita kutoka mautini kuingia uzimani. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy