... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uishi Katika Imani Yenye Ujasiri

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Habakuki 3:17,18 Maana mtini hautachanua maua, wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; taabu ya mzeituni itakuwa bure, na mashamba hayatatoa chakula; zizini hamtakuwa na kundi, wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe; walakini nitamfurahia BWANA, nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.

Listen to the radio broadcast of

Uishi Katika Imani Yenye Ujasiri


Download audio file

Laiti maisha yangekuwa shwari tu; ingekuwa tamu kabisa.  Laiti mambo yote yangeenda sawa sawa ili tuwe na afya, mali na hekima.  lakini bado kuna mafumbo na giza.  Sasa, mtu anawezaje kustahimili wakati wa kipindi kigumu?

Siku yenye giza kuliko zote ni wakati yale mema tuliyoyatazamia hayaonekani. 

Ni nani katikati ya furaha ya sikukuu yake ya arusi angetazamia kwamba baada ya miaka michache ndoa yake ingekuwa imeshaharibika?  Ni nani angetazamia kwamba mtoto mzuri aliyezaliwa leo siku moja angekuwa mvuta bangi, mtu anayetumia dawa za kulevya?  Ni nani katikati ya mafanikio yake kazini angetazamia kwamba, ghafla angepatikana na ugonjwa mkubwa? 

Kinachohitajika siku zile zenye giza ni mkakati wa kuweza kuvumilia na kuvuka kipindi hicho kibaya.  Sasa Mungu anao mkakati mwenye nguvu, hata kama unaonekana kwenda kinyume kabisa na mtazamo wa kawaida. 

Habakuki 3:17,18  Maana mtini hautachanua maua, wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; taabu ya mzeituni itakuwa bure, na mashamba hayatatoa chakula; zizini hamtakuwa na kundi, wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe; walakini nitamfurahia BWANA, nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.

Shida hazina budi kutokea.  Lakini katikati ya matatizo, tunaweza kuamua kuishi na imani yenye msimamo kidete, licha ya mazingira yetu.  Ni kwa sababu kupitia yote, tunaye Yesu – yule aliyekufa kulipa deni la dhambi zetu, akafufuka ili atupe uzima wa milele.  Na habari hii njema inatuletea ushindi katika hali zote zinazoweza kutokea maishani mwetu. 

Kwa hiyo, wakati kipindi kigumu kinakujia, chagua imani yenye ujasiri.  Amua kwa vyo vyote kumfurahia BWANA na kumshangilia Mungu wa wokovu wako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy