Ujazwe Roho
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 5:18-20 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Kuna mambo mengi mema ya kufurahia katika maisha haya. Na hata kama wengi wetu hatuishi daima kwenye “kilele cha mlima” kama wanavyosema, ni jambo bora kufurahia yale tuliyokirimiwa … lakini tusipite kiasi.
Kwanza, mimi nimejaliwa kupata mwanamke mwema kabisa na watoto watatu wazima na wajuguu watatu. Hawa watu saba wanakuwa baraka yangu kubwa katika dunia hii.
Nafahamu vizuri kwamba si kila mtu aliyebarikiwa hivi. Hata mimi niliwahi kuwa peke yangu katika dunia hii. Lakini haijalishi mazingira yako yakoje, bado kuna watu baadhi na vitu kadhaa ambavyo vinakuwa baraka kwako, si kweli? Kwa hiyo acha nitamke ikitoka moyoni kabisa kwamba ni sahihi tufurahie mema yaliyopo maishani mwetu.
Lakini hata hivi, kuna mpaka ambao hautupasi kuvuka katika swala hili. Hatari ni kwamba mtu anaweza, “kulewa” na vitu vya dunia hii, akaanza kuvihodhi kwa hali ya ubinafsi na uchoyo.
Waefeso 5:18-20 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Upendo ambao Mungu anakupenda pamoja na nia yake ya kukujaza na uwepo wake ni bora kuliko lo lote lile ambalo linapatikana katika dunia hii. Usiruhusu yaliyo mema maishani mwako yakuibie kilicho bora ambacho Mungu amekuandalia
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.