... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ujiweke Wazi Mbele za Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 51:6,7 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; nawe utanijulisha hekima kwa siri, unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

Listen to the radio broadcast of

Ujiweke Wazi Mbele za Mungu


Download audio file

Muda ule tunapotoka na kwenda njia mbaya, hvi huwa tunajua kama tumetenda yasiyo haki!, gafla tunakimbia na kujificha Mungu asituone.  Haieleweki kabisa, lakini ndivyo tunavyofanya.

Nadhani umeshapitia hali kama hiyo, hata mimi, unakuta silika zetu zinatusukuma kuficha makosa yetu huku tukitumaini labda Mungu hataona, lakini kumbe!  Kufanya hivyo ndo kwanza kunazidi kuleta uharibifu mkubwa!

Zamani, Mfalme Daudi aliiba mke wa mtu halafu aliagiza mtu yule auawe.  Mfalme wa Israeli alitenda uzinzi na akafuatisha mara moja mauaji.  Alijaribu kuficha dhambi yake na kufanya mume wa Yule mwanamke auawawe  vitani (na alikufa kweli akiwa vitani, na ni mfalme Daudi ndiye aliyepanga itokee hivyo).

Lakini kwa kutokana na upendo wake mkubwa, Mungu alimvuta Daudi kutoka kwenye hali hiyo kwa kutumia huduma ya Nabii Nathani.  Na kweli ilimshtua mpaka Daudi alijirudi.  Sasa, Zaburi 51 ni sala ya toba ya Daudi; dua ya kuomba Mungu atengeneze upya uhusiano wao.

Zaburi 51:6,7  Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; nawe utanijulisha hekima kwa siri, unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

Hapo hapo, Daudi anamwalika Mungu moyoni mwake.  Anamkaribisha Mungu aweze kuleta matengenezo, arejeshe ukweli wake moyoni ili aweze kujirudi kabisa.  Amfundishe pia hekima, amrudi na kumwosha awe safi.

Wakati tunatenda dhambi, hatuwezi sisi wenyewe kuweka mambo sawa.  Ni Mungu tu awezaye kufanya hivyo.  Jiweke wazi mbele zake ili uweze kupokea hekima yake, nidhamu yake pamoja na msamaha wake.  Usisite.  Kwa neema yake atakuweka sawa sawa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.