Ukristo Halisi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 6:1,2 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
Kuishi maisha yako yote ukijaribu kupendeza wengine na kujipendekeza kwao ni kazi ngumu kwa sababu watu ni wa kubadilika badilika. Wanaweza kuwa pamoja na wewe leo … lakini kesho wako kinyume. Bila shaka umeshashuhudia hayo.
Rafiki yangu mmoja wa karibu alikuwa mchungaji wa kanisa fulani miaka arobaini. Yeye na mke wake walijitolea sana kwa ajili ya watu, mimi nikiwemwo. Lakini baada miaka hiyo yote, rafiki zake wawili walimgeuka na kumpinga. Iliharibu kanisa lile. Pia, ilichukua miaka kadha yeye na mkewe kuponea tukio lile.
Kusalitiwa hivyo ni balaa, lakini hua inatokea. Inatokea kwenye sekta zote za maisha. Ndiyo sababu kubwa watu wengi wanajitahidi sana kupendeza watu wengine na kucheza kwa mpigo wa ngoma zao uliyo na kigeugeu.
Lakini kwenye ndoa imara, hakuna sababu kutafuta kupendwa na mwenzako. Tayari anakupenda. Unachokifanya sasa ni kuitikia upendo wake. Kuna utofauti mkubwa kati ya njia hizi mbili.
Na ndivyo ilivyo kwa Mungu. Hatubadilishi tabia yetu ili atupende. Tayari anatupenda. Tayari ameshamtuma Yesu kufa pale msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Bali, tunabadilisha tabia yetu kwa kuitikia upendo wake.
Warumi 6:1,2 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
Ukristo halisi ni mwitikio kwa upendo wake Mungu, si jitihada ya kuutafuta. Hii ni neema.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.