Umebarikiwa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 1:4-6 Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu.
Tuwe wazi. Kuna mara mambo hayaendi vizuri kama tunavyotaka … hata kidogo. Watu wengine wanaendelea vizuri tu. Wengine ni kama wanaona baraka katika maisha, ndoa zao, uchumi, na mengineyo. Lakini mimi? Wala!
Ni kweli, kuna wakati kila mmoja wetu anajihurumia. Ni kawaida wa mwanadamu kukatishwa tamaa mara kwa mara. Si vibaya isipokuwa hali hiyo ikiendelea sana. Kama mtu daima ana mtazamo hasi, akisononeka na kunung’unikia wanaomzunguka, ni hatari. Hakuna mema yanayoweza kutokea!
Ikiwa unashikwa na mtazamo kama huo, mara nyingi ni kwa sababu mazingira yako yanakulemea kama vile wingu jeusi au ukungu mzito na kuzuia jua lisikuangazie, hata kama jua bado linawaka pale pale.
1 Wakorintho 1:4-6 Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu.
Neema ya Mungu kwako kupitia Yesu – kama kweli umeweka tegemeo lako kwake – kamwe haiwezi kuyumba-yumba. Haipungui. Si kwamba ipo leo wakati mambo yako shwari halafu inatoweka kesho wakati mambo yanakuwia vigumu, hapana.
Halafu ndani yake yeye umebarikiwa kwa njia zote. Njia gani? Katika usemi, katika maarifa … katika mambo yote.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.