... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Umepewa Vitu Vingi Sana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:7 Hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Umepewa Vitu Vingi Sana


Download audio file

Kuna watu baadhi wanapenda sana kupokea zawadi – ndivyo walivyoumbwa.  Ni njia inayowapendeza zaidi kwa kupokea upendo na kujenga urafiki.  Wengine sio sana.  Wewe vipi?  Unapenda kupokea zawadi au si sana?

Kama unapenda sana kupokea zawadi, ni vizuri. Si vibaya hata kidogo.  Mimi binafsi, sijali kama nitapata tena zawadi siku ya kuzaliwa kwangu au wakati wa Krismasi kwa miaka ninayobakiza hapa duniani.  Sijali kabisa.

Lakini hata kama ndivyo nilivyo, kulikuwa kipindi maishani mwangu wakati sikuwa na kitu – yaani nilipoteza kila kitu, vyote viliniharibikia.  Ndipo nilijaliwa kupata zawadi kubwa kuliko zote.  Zawadi iliyobadilisha maisha yangu.  Mtume Paulo aliwaandikia hivi watu wa kanisa la Korintho zamani kwenye karne ya kwanza:

1 Wakorintho 1:7  Hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.  

Akisema “hamkupungukiwa karama yo yote” anamaanisha nini?  Jibu ni kwamba tuna kila kitu kinachohitajika, vyote ambavyo ni muhimu kwetu kwa maisha.  Hekima, vipawa, neema yake Mungu, upendo wake, Roho yake kukaa ndani yetu kadiri tunavyomwamini Yesu.  Kila karama … kila zawadi.

Kwa hiyo hata yule ambaye kwa mtazamo wa dunia ni maskini wa kutupwa … wakati anamwamini Yesu, ana kila kitu, kila zawadi.

Sote tutulie kwanza na kutafakari ahadi hiyo, tutafakari ukweli huo.  Karama yo yote, kila zawadi.  Ni mali yako kama umemwamini Yesu.  Na wewe pia vinakungojea kama unataka kumwamini Yesu sasa.

Karama yo yote.  Ni ahadi ya Mungu.  Ni kweli yake.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy