Unasimama Wapi?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 19:25,26 Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, mama, tazama, mwanao.
Sijui kama umeshaona jinsi maisha yakiendelea shwari, unao watu wengi walio karibu yako, lakini wakati mambo yanaanza kukuharibikia, wengi wao wanatoweka?
Hii isingetushangaza. Kwa sababu wakati mambo yanaanza kuwa magumu, ni kawaida mwanadamu kujaribu kukimbilia sehemu ya starehe na usalama. Ni wachache mno wako tayari kukabiliana na matatizo yanayokukumba wewe.
Kwa hiyo swali inakuja: Je! Wewe ni mtu wa aina gani? Uko tayari kusimama kidete licha ya magumu, au uko mtu atakayekimbia wakati wa matatizo?
Zamani, wakati Yesu alikuwa anatenda miujiza ya ajabu-ajabu, watu maelfu walimkusanyikia. Yaani mji mzima uliweza kufunga kazi na kutoka kumkuta kwenye mbuga za malisho ili wamsikilize akifundisha.
Hatimaye alichagua watu kumi na wawili kati yao kukaa karibu naye. Halafu kati ya hawa, ni watatu tu waliweza kumkaribia zaidi kwenye bustani ya Gethsemane kwa maombi usiku ule aliosalitiwa. Halafu kesho yake, ilikuwa hivi:
Yohana 19:25,26 Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, mama, tazama, mwanao.
Msalabani pale, kulikuwa wanawake wanne (mmoja alikuwa mamaye) na mwanafunzi mmoja tu. Sasa, wale wengine maelfu, au hata wale kumi na wawili walikuwa wapi?
Ukweli ndo huu: Kadiri mtu anakaribia Msalaba, ndipo ataona kwamba watu wanazidi kupungua. Kwa hiyo niulize, Je! Wewe unasimama wapi?
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.