Unifundishe
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 143:10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa.
Ni kama kuna aina mbili za watu duniani. Kuna wenye mioyo inayofundishika, na kuna wenye mioyo isiyofundishika. Kuna watu wako tayari kukiri makosa yao na kujifunza kwayo ili waweze kuboresha maisha yao … na kuna wale wanaoshindwa kujifunza lolote.
Kwahiyo … Utaniruhusu nikuulize, je! Wewe ni mtu wa aina gani? Usijibu haraka, tafakari kwanza, usijidanganyike, kwasababu moyo wa mwanadamu huwa na tabia ya kujidanganya.
Ebu jaribu kukumbuka mgogoro uliowahi kuwa na mtu mwingine hivi karibuni. Je! Hatimaye, ulikubali kwamba kwa sehemu, ghasia hii umeileta mwenyewe au uliiongeza angalau? Au ulimshutumu yule mwingine tu?
Je!, Ulimuomba Mungu akuonyeshe namna ya kusamehe, jinsi ya kufanya ili isitokee tena, au ulifunika tu tukio lote ili uweze kupigana naye tena siku nyingine? Maswali hayo ni changamoto, sindiyo? Sasa, wakati unayatafakar hayo, sikiliza alivyoomba mtumishi mwingine wa Mungu aliye Hai, akipambana na changamoto kama hizo:
Zaburi 143:10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa.
Huyu ni Mfalme Daudi, aliwindwa na adui yake, aliyepondwa hadi chini na kulazimishwa akae gizani kama vile waliokufa zamani (angalia mstari wa 3 wa Zaburi hii hii). aliombaje? Seta adui yangu, umwangamize, Eeh Mungu? Wala. Alikuwa mwenye busara, kwa hiyo asingeweza kuomba hivyo.
Daudi alifahamu kwamba cha muhimu katikati ya mazingira yale magumu, kilikuwa ni kugundua mapenzi ya Mungu na kumruhusu Roho Mtakatifu amwongoze aende mbele kwenye tambarare.
Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.