... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uovu Utaisha Lini?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 25:46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Listen to the radio broadcast of

Uovu Utaisha Lini?


Download audio file

Tukizingatia yanayoendela duniani, wengi wetu tunajiuliza – Je!  maovu hayo yote yataisha lini?  Hili ni swali zuri linaloeleweka. Yataisha lini?

Kwanini Mungu wa upendo anaruhusu vita nyingi kuendelea wakati wasio na hatia wengi wanauawa, wakiwemo watoto wanaokufa, au kulemazwa na kumezwa na kiwewe?  Kwa nini matajiri wanazidi kutajirika duniani na maskini kuzidi kuwa na hali duni?  Kwa nini Mungu anaruhusu mtu huyu mmoja anayesumbua kuendelea na ukorofi wake?  Kwanini asikanyage uovu kama kweli yeye ni Mungu wa upendo?

Lakini wengi kati ya hao wanaouliza maswali kama hayo, hawataki Mungu awaambie lolote hasa linalokwaza  hisia zao.  Wanafikiri pia kwamba Wakristo wanaoongea habari za mbinguni na jehanamu, dhambi na haki; kwamba hawako sahihi!

Lakini kama mtu anapendelea kuwa na Mungu asiyehukumu, basi atabaki na uovu.  Kama unataka uovu ukomeshwe, lazima ukubali Mungu atakayehukumu kwa haki.  Ndio maana Yesu mwenyewe alisema hivi:-

Mathayo 25:46  Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Kwakweli, habari za haki ya Mungu, hukumu zake na adhabu ya milele zinawangojea wanaokataa mada ya Yesu.

Huwezi kutaka uovu uondoke bila hukumu kuwepo.  Kama kweli unataka uovu ukomeshwe, lazima ukubali kwamba Mungu atauhukumu.  Ndipo waovu watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele.  Ndipo uovu utakuwa umeisha kabisa.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy