... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Upendo Usio na Makona

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 13:8-10 Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

Listen to the radio broadcast of

Upendo Usio na Makona


Download audio file

Mtu akiangalia uovu unaotuzunguka, lazima ajiulize, je!  Dawa itapatikanaje?  Suluhisho linaweza kutoka wapi?  Tunawezaje kuuzuia?

Wanaume wasio waaminifu kwa wake zao wakizini, wanawake kutokuwa waaminifu kwa waume.  Ujeuri, mauaji, uongo, uchoyo, wivu.  Tukiwa wazi, hata wewe na mimi tunayo hatia katika baadhi ya mambo hayo.  Naamini hatuzami katika maovu, lakini bado tunawafokea watu, bado tuna wivu, tunajitanguliza, tunakosa adabu … na mengineyo.  Tukisema ukweli, sisi pia tunasababisha uovu utokee.

Kwa hiyo, turejee swali lile, je!  Mtu angefanyaje ili azuie uovu?  Kumbe!  Jibu linapatikana kwa urahisi kuliko tunavyoweza kufikiria.

Warumi 13:8-10  Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.  Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.  Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

Je! ni kweli, jibu linaweza kuwa rahisi hivyo?  Ndiyo inawezekana.  Ukiamua kumpenda aliye karibu yako – yaani “jirani” yako kama alivyosema Mtume Paulo – mara moja mchango wako katika uovu unastopishwa.

Sasa majirani wale labda wataonekana tofauti na wewe, hata msemo wao unaweza kuwa tofauti, imani tofauti, mienendo tofauti; hata kukusumbua mara kwa mara.  Hata hivi uwapende kwa sababu maovu hayawezi kuendelea wakati mtu anampenda jirani yake kama nafsi yake.

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy