... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Upuzi wa Msalaba

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:18,19 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa.

Listen to the radio broadcast of

Upuzi wa Msalaba


Download audio file

Naweza kukuuliza leo, je!  Una akili kiasi gani?  Ukiangalia nyuma katika maisha yako, je! Umefuataje njia ya hekima?  Pengine umefaulu vizuri.  Lakini pia, nadhani umetoka ndani ya ile njia zaidi ya mara moja, kama nilivyofanya mimi, na tumekula hasara, si kweli?

Kuna wakati hekima inaonekana kuwa na kigeugeu.  Hekima yangu inakuwa tofauti na hekima yako – ni kwa sababu tuko watu wawili tofauti waliopitia mambo tofauti-tofauti, katika mazingira na utamaduni tofauti.

Halafu kwa kuwa hekima hua inakua taratibu kupitia matokeo mbali mbali, inawezekana kwamba wewe na mimi tunayo mitazamo tofauti kabisa kuhusu jinsi ilivyo.

Kama ungaliniuliza kuhusu hekima yangu nikiwa kijana wakati ule, kukadiria kwa maksi fulani kuanzia sufuri hadi kumi, ningejipa maksi ya 8 au 9 … na hii ni dalili kwamba sikuwa na hekima, bali nilijaa kiburi tu. Niligundua hekima nyingine iliyobomoa hekima yangu ya kidunia: 

1 Wakorintho 1:18,19  Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.  Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa.

Hata kama tunajiona kuwa na hekima kiasi gani, hata kama tulikuwa tunadhani kwamba Ukristo ni upuzi tu, hekima ya Msalaba wa Kristo, dhabihu Mungu mwenyewe alitoa kuokoa watu kama wewe na mimi, ni nguvu, ni nguvu pekee iwezayo kutuokoa na ubinafsi hadi milele.

Yesu ni wa kipekee kila kitu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy