Urafiki Wako na Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 5:9,10 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.
Sikukuu ya Krismas ambayo tutasherehekea baada ya siku chache, ni sherehe ya familia na rafiki, chakula kitamu na mapambo mengi. Lakini kumbe! Kuna rafiki mmoja ambaye mara nyingi, tunasahau kumwalika mezani.
Je! Umewahi kusalitiwa na rafiki yako? Ni jambo linalohuzunisha mno. Naweza kukwambia kwamba kovu kubwa nililo nalo lilitokana na kusalitiwa na rafiki. Yaani ilichukua miaka mingi sana, jeraha hilo kupona … na hadi leo, kovu lile limebaki kuwa sehemu ya maisha yangu.
Kwa kweli, sisi sote tumemsaliti Mungu – katika mawazo yetu, maneno yetu na matendo yetu. Kwa hiyo, ili aweze kuponya mahusiano, Yeye mwenyewe alijiingiza katika ulimwengu wetu, aweze kubeba kovu zetu. Kama vile tulivyoweza kuangalia jana …
Warumi 5:9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
Kama vile nabii Isaya alivyoandika miaka mingi iliyopita, kupitia jeraha zake, sisi tumepona. Kwa sababu gani? Lengo kuu la Mungu lilikuwa nini?
Warumi 5:10 Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.
Lengo lake Mungu lilikuwa hivi, na bado analo leo, kwamba atupatanishe naye; atulete karibu; aweke daraja kwa kumfikia kwa kufuta dhambi zetu kupitia dhabihu ya Kristo pale msalabani … Ili tuweze kuwa rafiki zake.
Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake. Tafadhali, usisahau kumwalika Rafiki huyu akae mezani kwenu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.