Ushangae
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mariko 1:21,22 Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha. Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi.
Sijui umekaa kanisani siku ngapi mpaka leo, lakini mimi siwezi kuzihesabu kwa kuwa ni nyingi. Mimi nilianza nikiwa mtoto mdogo. Kukaa kimya saa nzima; kusema ukweli iliniumiza sana. Kwangu mimi mahubiri yalikuwa hata hayanivutii kabisa.
Ni kweli, nilikuwa mtoto tu na pengine kule kuchoka kulitokana na hali ya utoto. Lakini siku hizi, tukiwa na teknolojia mikononi mwetu, tuna nafasi kubwa ya kupata mafundisho ya Kikristo … lakini bado kuna mahubiri mengi yanayohubiriwa huku yakikosa nguvu.
Hotuba zisizosisimua siku hizi ni jambo kawaida; au mhubiri kupiga kelele masikio mwetu kwa kuongea maneno tuliyotamani kuyasikia; bila ya kuwa na uwezo wa kubadilisha maisha yetu, nikawaida na wala haikuanza leo.
Mariko 1:21,22 Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha. Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi.
Je!, Ni lipi lengo ya mahubiri? Sijui kama umeshajiuliza swali hilo. Lengo ni kufikisha Neno la Mungu mioyoni mwetu, Neno la milele liwezalo kutupindua na kutubadilishia maisha. Lengo ni mabadiliko katika maisha yetu. Lengo ni kutufanya tujikane na kuchukua msalaba na kumfuata Yesu. Hilo ndilo lengo, kwahiyo tafuta mahali pale ambapo mahubiri yanauwezo wa kukugusa hivyo.
Angalia, kama hutaki kuletewa changamoto na maisha yako; kupinduliwa, basi Jumapili asubuhi nenda ukacheze mpira. Lakini kama uko makini, basi unahitaji mtu anayefundisha kwa amri kama YESU.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.