Usifanye Kosa Hili
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 3:2 Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.
Wakati tunaangalia nyuma kwa yale yaliyopita, wewe na mimi tunaweza kukumbuka wakati tulinena maneno yaliyowaumiza watu Uongo, Dhihaka na kadhalika maneno ambayo yaliwaumiza moyoni.
Ni dhana yenye tafakuri Kwamba wewe na mimi tumeumiza watu maishani mwetu; kwamba tumeacha uharibifu pale tulipopita kwa maneno tuliyoyawaambia watu wengine.
Niliwahi kusikia mtu fulani akisema kwamba maneno ni kama machupa yanayobeba uwezo. Na ni kweli. Yale tunayoyasema na tunayotamka, yote mawili yanabainishia ni jinsi gani unamfikiria mtu mwingine.
Madhara yaliyosababishwa na maneno yetu, yanadumu maisha yote.
Yakobo 3:2 Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.
Ni ajabu kabisa! . Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu … mkamilifu!
Lakini kwa muda huu, jua hili: maneno yana nguvu ya kujenga au nguvu ya kubomoa. Kila neno tunalolinena, wewe na mimi, kwa sehemu, litatenda kimoja au kingine.
Uwe mwangalifu kwa yale unayotamka.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.