Usikwazike
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wagalatia 6:2,3 Mchukuliana mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.
Wakati watu wengine wanatutendea visivyo, ni rahisi sana kukwazika mara moja. Tukisema ukweli, ulimwenguni humu watu wanazidi kudai “haki” zao na mwitikio wao wa kwanza ni kukwazika.
Lakini tunagalie kwanza na kutafakari jinsi sisi wenyewe tumetenda visivyo, wewe na mimi. Ni yapi yamesababisha tutende hivyo? Inawezekana ilitokana na mambo mbali mbali. Labda kuna jambo lililotonesha maumivu ya zamani, jeraha tulokuwa nalo moyoni.
Pengine tunasongwa na mambo mengi kama inavyotokea duniani, kwa hiyo tunafokea wengine. Au labda ni kwa sababu watu wenye upungufu wanatukosea tu.
Sasa, sababu hizo hazitulengi sisi tu, wewe na mimi lakini zinalenga wanaotuzunguka pia, wakienenda vibaya mara kwa mara. Yaani hatuwezi tena kukwazika mara moja sababu tunajua kwamba na sisi tunakwaza wengine pia. Yamkini kuna njia mbadala.
Wagalatia 6:2,3 Mchukuliana mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.
Kwa hiyo, mtu anaweza kuendelea kukwazika au anaweza kusaidia watu wale katika matatizo walio nayo – mambo yanayowachokoza, mapungufu yao, madhaifu waliyo nayo – kwa njia ya kuacha kwanza kuhukumu na kujaribu kuwaelewa.
Angalia, watu kwa wastani si wabaya. Mienendo yao mibaya yanatokana na kitu kingine. Kilicho kibaya ni kujiinua na kuwahukumu na kukwazika haraka. Mtazamo kama huo ni mbaya.
Kama vile mtu fulani alivyosema, si kwamba mtu akusudie kufitina wengine ile aathiri watu wengine. Kuacha tu kuchukuliana nao na kujaribu kuwaelewa inatosha kwa kuwaathiri.
Mchukuliana mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.