... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usipotoshwe

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Yohana 3:7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki.

Listen to the radio broadcast of

Usipotoshwe


Download audio file

Kukutana na watu wapya, kujenga urafiki si rahisi siku hizi.  Maisha yamekuwa bize kupita kiasi, watu wakikutana kikazi tu, au kwa wengine, maisha yamekuwa ya upweke kabisa.  Lakini usihofu, teknolojia imeleta jibu.

Tovuti za kukutanisha wanaume na wanawake zimetengenezwa miaka michache iliyopita, lakini tayari kuna watu nusu-biliyoni wanatumia tovuti zile ambazo zimeingiza mapato ya dola za kimarekani ma-bilioni ma-mia kila mwaka. 

Unajua, inazidi kuwa vigumu kwa watu, vijana kwa wazee, kukutana na watu wengine na kujenga mahusiano mazuri.  Labda ni kwa sababu watu wengi wanachukua muda mrefu wakizamisha nyuso zao kwenye skrini ya simu janja.

Kwa vyo vyote, badala ya kujaribu kujiingiza kwenye kundi la marafiki, au kujiunga na kanisa fulani … wanatafuta-tafuta urafiki mtandaoni.  lakini, mtu hawezi kuwa na uhakika kwamba ataweza kujenga urafiki wa kweli kwa njia hiyo.

1 Yohana 3:7  Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki.

Kama vile mhubiri wa karne ya 17 aitwaye Thomas Brooks alivyosema, “Marafiki zako wa karibu wawe wale waliomfanya Kristo kuwa rafiki yao wa kwanza.”  Ina maana, uwe makini sana ukichagua marafiki.  Chagua wale ambao watakushawishi kumwelekea Kristo ili hatimaye utende yaliyo haki.

Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy