... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usipuuze Taarifa ya Kweli

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 17:14-17 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lake ndiyo kweli.

Listen to the radio broadcast of

Usipuuze Taarifa ya Kweli


Download audio file

Wakati Pontio Pilato anasimamia kesi ya Yesu mahakamani aliuliza swali, “Je!  Kweli ni nini?”  Ni swali ambalo hata mimi huwa nauliza kila siku.  Nadhani ni muhimu tuliulize ili tusepelekwe na mafuriko ya uongo yaliyoenea kila kona.

Labda ninaonekana kama mmoja wa wale wanaofikiri kila jambo ni njama za watu, sindiyo?, lakini kutilia mashaka mambo ambayo wengine wanatetea kuwa NI kweli, ni jambo lenye busara. 

Aldous Huxley, mwanafalfasa Mwingereza wa karne iliyopita, mtu ambaye aliyekiri wazi kwamba yuko kinyume na Ukristo, lakini hata hivyo alisema yafuatayo:  Kanuni au taarifa za kweli, hazitoweki kwa kuwa watu wanazipuuza. 

 Ni dhana aliyoieleza vizuri sana kwenye kitabu alichoandika kiitwacho, “Brave New World” yaani, “Ulimwengu Mpya wa Ushujaa”.  Kumbe, shujaa wa kweli ndani ya hadithi ni mtu aitwaye Bernard Marx, yeye peke yake aliweza kusimama kidete na kutilia mashaka na kuleta hoja kuhusu mbinu za kubadilisha jamii ambazo zilikuwa zinaendelea wakati ule.  Hatimaye alifukuzwa nchini na kutupwa kwenye kisiwa kwa sababu hakupatana na mfumo wa utawala huo. 

Kusimama kidete kutetea ukweli hakujawahi kupendwa na wengi.  Muulize Yesu.  Walimsulubisha kwasababu alitetea kweli.  Maneno yafuatayo ni dua aliyowaombea wanafunzi wake kuhusu kweli: 

Yohana 17:14-17  Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.  Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.  Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.  Uwatakase kwa ile kweli; neno lake ndiyo kweli. 

Kweli siku hizi inapatikana kwa nadra sana – ikiwa kwenye vyombo vya habari, kwenye tovuti za jamii au katika siasa.  Pia ni vigumu kuiona kweli kwenye tabia za watu ambao maadili yameporomoka sana.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy