Usitegwe
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 29:25 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.
Wazo la kushikwa na mtego aina yo yote linatisha kweli. Ebu fikiria kama ungefungiwa ndani ya chumba katika meli inayozama baharini. Au fikiria kuwa umetumbukia ndani ya machimbo mahali fulani. Ebu fikiria …
Samahani kwa kuwa nimeanzia na maneno yanayotisha, uniwie radhi. Lakini ukweli ni kwamba watu wengi leo wanajikuta ndani ya mtego kwa njia moja au nyingine. Yamkini kuna jambo fulani katika mazingira yako muda huu ambao linakuletea hisia kwamba umeshikwa ndani ya mtego fulani.
Kipindi cha janga la korona wakati wengi walifungiwa ndani, nilihurumia akina mama na watoto pia ambao walifungiwa pamoja na wanaume katili – jinsi ilivyowaathiri.
Lakini kuna wakati ni sisi wenyewe tunajitengenezea mitego. Ni kama sisi wenyewe tunajifungia ndani na kupoteza funguo.
Mithali 29:25 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.
Anachotwambia Mungu katika mstari huu ni kwamba woga wenyewe ni mtego. Watu wanahofu kwa sababu hawaoni jinsi ya kutoka kwenye ajira yao mbaya, au katika magonjwa yanayotisha yasiyo na tiba.
Kama tunajisikia kuwa ndani ya mtego kwa sababu ya matukio yale, au kama tunajisikia huru kama ndege licha ya matatizo yale, itakuwa inatokana na jinsi mtu anakabiliana na hofu … na kama atakuwa ametumia dawa yake.
Kama daima unakiri kwamba uko peke yako, basi hofu itakuwa kama mtego kwako – yaani gereza ulilotengeneza wewe mwenyewe.
Bali ukimtumainia BWANA utakuwa salama.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.