... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Utukufu wa Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Listen to the radio broadcast of

Utukufu wa Mungu


Download audio file

Jua ikiwaka vizuri inasisimua mtu, si kweli?  Sijui kama umewahi kujiuliza kwa nini?  Kwa nini tunapendelea jua kuliko mvua; upepo mwanana badala ya upepo wa baridi?

Jambo kubwa kwetu kwa mtu anayetaka kununua nyumba, ni kuangalia nuru ya asili inatokea wapi.  Kama unaishi kusini sana mwa ikweta, inatakiwa sebule inangalie kaskazini.  Kama unaishi kaskazini sana mwa ikweta, inatakiwa sebule iangalie kusini.

Mimi na mke wangu tulichangia chakula na marafiki hivi karibuni na walikuwa wanatusimulia jinsi mzazi wao mmoja mzee alikuwa anahama-hama kutoka chumba kimoja kuelekea kingine mchana akifuata mwelekeo wa jua.

Kwa nini tunapendelea nuru?  Sijui lakini ndivyo tulivyo!  Na bila shaka, siku zenye giza na dhoruba maishani, wakati mambo hayaendi vizuri kama tulivyotazamia, kupata nuru nusu angalau, ingependeza sana, si kweli?

Na ni kwa maana hiyo kabisa Yesu alikuja hapa duniani … kwa ajili yako.

Yohana 1:14  Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Yohana anamtaja Yesu kuwa “Neno” – logos kwa lugha ya asili ya Kiyunani.  Mungu akinena nasi kwa kufunika utukufu wake ndani ya mwili wa mwanadamu, utukufu halisi wa Mungu Mwenyewe, nuru inayoshangaza kupita jinsi ingeweza kuelezwa kwa maneno.

Mungu alikuja ili wewe na mimi tuweze kuona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Mungu, amejaa neema na kweli.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy