Uukumbatie Mwaka Mpya Ulioanza
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 4:13-15 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, nakufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
Je! Mipango yako kwa ajili ya mwaka mpya ni ipi? Je! Ni mipango mizuri ambayo inachangamsha hisia zako moyoni? Au labda kuna hofu na mashaka yanayokuletea mafumbo tu?
Mtu akitafakari kidogo, ataona kwamba kuna aina mbili za mipango mtu anaweza kuwa nayo; mitazamo miwili ya mambo yajayo. Kuna mipango ya kujenga ambayo tunaweza kuianzisha kwa moyo mkuu na bidii, halafu kuna mipango hasi kabisa, wakati mashaka yetu yanazidi kutuletea hofu.
Lakini kuna kipindi mambo hayaendi kama tulivyotazamia. Mipango yetu mizuri inaweza kutuharibikia. Pia yale mabaya tulioyohofia, kumbe! Hayatokei. Sasa, kwa kuwa hakuna uhakika, mtu atawezaje kukumbatia mwaka huu unaokuja? Mtu atajiandaaje ili awe na mtazamo wenye uhalisia utakaoweza kukabiliana na cho chote kile kinachotokea katika maisha? Kuna jibu …
Yakobo 4:13-15 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, nakufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
Kwa maneno mengine anasema usitegemee akili zako. Usijidai sana wala usikatishwe tamaa haraka kwa yale unayofikiri na kuyaona, bali yaweke yote miguuni pake Mungu. Yeye anayajua yote. Yeye daima ni mwaminifu. Anakupenda kuliko jinsi ungeelezea.
Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au vile.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.