Uungojee Msaada Wake
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 30:18 Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
Zamani wakati nilikuwa jeshini, tulikuwa na msemo, “Wahi upate kusubiri.” Ni kama walituwahisha kwenda sehemu tusichelewe, lakini baada ya kufika eneo husika, tulisibiri masaa mengi kuona kitakachofuata.
Kule “kuwahi upate kusubiri” hua kunatokea mara nyingi maishani pia. Mtu anabanwa awahi kwenda sehemu au kutimiza jambo fulani … halafu mazingira ambayo yako nje ya uwezo wake yanakwamisha yote na kusababisha yaende pole pole.
Katika ulimwengu wetu wa kidijitali na kuwa hewani kwenye utandawazi masaa 24 kila siku ya wiki, tunatazamia mambo yatokee papo hapo. Je! Unajisikiaje ukisubirishwa nusu saa wakati unapiga simu kwa huduma kwa wateja? Nadhani unanielewa. Hatuna tena subira siku hizi.
Lakini kwa sababu ambazo zinaeleweka kwake yeye tu, Mungu anathamini sana uvumilivu na subira. Si kusubiri kwa basi tu tukinung’unika wakati tunasubirishwa, lakini ni kujifunza subira iletayo uvumilivu na kujenga moyo wa matumaini ndani yetu.
Isaya 30:18 Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
Kwa hiyo, tukisubiri jibu la ombi letu, ujue kwamba na yeye Mungu anasubiri pia. Anangoja aweze kutuonee huruma. Ana shauku kusimama na kutufariji. Sasa, anasubiri nini?
Hatuwezi kujua hakika, lakini mimi ninadhani kwamba anasubiri muda mwafaka. Muda wake mwenyewe, muda mioyo yetu itakuwa imetulia ndani yetu. Atatenda yaliyo haki kwa muda ufaao. Atabariki kila mtu anayeungojea msaada wake.
Kwa hiyo … uusubiri.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.