Uwezo Ndani ya Maswali
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 19:16-18a Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. Akamwambia, Zipi?
Laiti maisha yangekuwa sahili … lakini sivyo ilivyo. Maisha mara nyingi ni ya fujo, ni gumu kufahamika. Hisia za watu, zetu zikiwemo, ni kigeugeu. Mara nyingi tunakabiliana na mazingira yenye utata. Kwa kweli, maisha si sahili.
Ni lini mtu aliwahi kukusumbua au hata kukuumiza wakati alileta jibu laini au kutumia maelezo chapwa wakati ulikuwa unakabiliana na swala gumu mno? Je! Jibu lake lilikugusaje?
Mara nyingi Yesu alikabiliana na hoja zenye ubishi.
Mathayo 19:16-18a Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. Akamwambia, Zipi?
Swali nzuri tu. Yesu alijibuje? Alileta swali lingine, lililosababisha majadiliano mapana yanayohusu swali la msingi linalolenga uzima na mauti. Unajua, nimeambiwa kwamba katika Injili nne zinazosimulia habari za maisha yake – Mathayo, Mariko, Luka na Yohana – Yesu aliulizwa maswali 187. Alijibu kama nane tu. Yeye mwenyewe aliuliza maswali 307. Mara nyingi alitoa mifano ambayo watu hawakuelewa. Bila shaka walirudi nyumbani wakisemezana, “Wewe, unawaza alikuwa na maana gani?”
Kuna uwezo mkubwa katika kuuliza maswali – tukijiuliza sisi wenyewe, tukiwauliza watu wengine, tukiwa na maswali yahusuyo Neno la Mungu. Ni tabia nzuri kwa kupanua mawazo na kuchochea fikra za mtu na kukaribisha watu waweze kujadili mada fulani.
Usiogope kuuliza maswali.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.