Uwezo Utokao Juu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 40:28-31 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Wanasema uwezo wa mamlaka unapotosha, na uwezo wote unapotosha kabisa! Si lazima mtu aangalie mbali ili aone kwamba hii ni kweli kabisa na akiangalia mbali zaidi atashuhudia kwamba ulimwengu wetu umevurugika kwa sababu ya madikteta.
Hata makanisani kuna watu wanagombania madaraka. Kwa hiyo isitushangaze kuona jinsi watu wengi wanachukizwa na dini. Isitushangaze kwamba wengi wanamtilia mashaka hata Mungu. Hatuwezi kuwalaumu wakati tunakumbuka maovu yaliyotendeka kupitia makarne mengi na hata siku hizi kwa jina la dini!
Lakini juu kabisa ya maovu hayo yote yaliyotendeka makarne na makarne, kuna Mungu anayetaka kuwawezesha watu wa kawaida kama wewe na mimi kutokana na pendo lake halisi, akitukirimia uwezo wake usio na mipaka. Tumsikilize tena akiongea na watu wake waliokuwa wameteswa vibaya karibia miaka sabini:
Isaya 40:28-31 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Rafiki yangu, ninaamini na moyo wangu wote kwamba ujumbe huu ni kwa ajili yako leo hii, mahali ulipo. Wakati unataka kuzimia, wakati unaishiwa nguvu, umgoje Mungu. Umtegemee Mungu. Umtumainie Mungu. Naye atakupa nguvu mpya. Atakuinua na uwezo wako. Ni kweli kabisa!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.