... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwezo wa Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 1:12,13 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Uwezo wa Mungu


Download audio file

Leo ni siku ya kuamkia Krismasi.  Ni muda wa kutafakari na kujiuliza swali.  Kwa sababu siku ya leo inadai jibu la swali hili:  Je!  Kesho nitasherehekea nini?  Je!  Ni mapokeo ya familia au ya dini, au kuna zaidi?

Kwa kweli, mimi siwezi kujua mawazo yako ya leo yahusuyo Krimasi; kama unaamini au la…

Jana tulisimulia ukweli kwamba watu wengi sana wamemkataa Yesu, au kwa makusudi au kwa kumpuuza tu; au kwa kufikiri kwamba habari zake zote ni hadithi tu … au kwa kuzembea no kutokumjali wala kujali kazi aliyokuja kuifanya.

Labda ndivyo ulivyo … au pengine wewe ni mtu ambaye tayari umeshakabidhi maisha yako kwake Yesu; mtu ambaye moyo wako umejaa furaha tele ukisikia jina lake likitajwa tu.

Popote ulipo, dua langu ni kwamba uruhusu maneno yafuatayo, ambayo ni Neno la Mungu, yakumulikie moyoni leo hii:

Yohana 1:12,13  Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Mara tu unapomkubali Yesu, papo hapo unakuwa mtoto wa Mungu na mambo yote – mambo yote kabisa – yanabadilika … kuanzia sasa hadi milele zote.  Ukweli huu ukusaidie kujibu maswali uliyo nayo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy