Uwezo wa Neema ya Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 1:16,17 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
Acha nikuulize … neema ni nini hasa? Kwa wengine, ni neno la kidini linalotumika sana hadi linapoteza maana yake. Lakini neema ni nguvu pekee yenye uweza mkubwa kuliko vyote vinavyoweza kubadilisha ulimwengu.
Jana tulisherehekea Sikukuu ya Krismasi. Tuliona kwamba Mungu alitaka kuongea nasi kupitia huyu Yesu, Mungu Mwana, aliyemtuma kufanyika mwanadamu na kukaa hapa, katikati yetu:
Yesu, aliye Neno la Mungu, yaani Mungu akiongea nasi kwa kutumia lugha tunayoielewa, akimulikisha utukufu wake juu yetu, akimwaga neema na kweli yake maishani mwetu. Halafu kwa mistari ifuatayo :
Yohana 1:16,17 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
Torati, yaani dhana ya kufuata orodha ya amri mbali mbali, haiwezi kumbadilisha mtu. Lakini neema – yaani karama inayotolewa, kuonyesha fadhili na msamaha ambao mtu hastahili … kwa kweli, inaweza kumbadilisha anayevipokea.
Hakuna hata mtu mmoja anastahili Yesu – si wewe, si mimi. Kifo chake pale Msalabani ili alipe gharama iliyodaiwa na haki yake Mungu kwa sababu ya uasi wetu, hatustahili. Lakini Mungu alitukirimia neema juu ya neema, karama inayotolewa bure ya kuleta msamaha kupitia Yesu pamoja na uzima wa milele, yote yanatokana na pendo lake kuu kwako wewe na kwangu mimi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.