... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wakati Biliyonari Anafariki Dunia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 1:9-11 Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa; bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka. Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

Listen to the radio broadcast of

Wakati Biliyonari Anafariki Dunia


Download audio file

Ulimwengu kwa ujumla, umetawaliwa na tamaa ya mali, si kweli?  Pesa, pesa, pesa.  Nawezaje kupata zaidi?  Nawezaje kongeza mapato angalau kidogo ili niweze kununua vitu vyote vya anasa ninavyotamani?

Waandishi wa habari mara nyingi wanapenda kutoa ripoti tujue ni yupi tajiri kuliko wote duniani.  Je!  Ni Elon Musk wa kampuni ya Tesla, au Jeff Bezos wa Amazon, au ni Larry Ellison wa Oracle, au Warren Buffet, au Bill Gates?  Wote ni wanaume ambao utajiri wao unapimwa kwa ma-bilioni ma-mia ya dola za kimarekani; yaani kwa viwango ambavyo sisi watu wa kawaida hatuwezi kuanza kuvielewa.

Ni kama hawawezi kuguswa, wakikingwa na utajiri huo mkubwa, ni kama hakuna kingeweza kuwaathiri.  Lakini hii sio kweli hata kidogo.

Yakobo 1:9-11  Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa; bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka.  Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

Mali sio kinga ndoa yake tajiri isiharibike au mtoto wake kuwa kaidi.  Haiwewi kumfanya asiwe na huzuni wala asifadhaike.  Mali haiwezi kulinda mtu asipate misiba inayomshusha.  Halafu kamwe, mali haiwezi kumlinda asife.

Tafadhali sana, usiruhusu kamwe mali uliyo nayo ikudanganye kwamba uko salama salamini, kama vile wanavyofanya matajiri wengi.  Vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.   

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy