Wakati Pendo Linashinda
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 3:18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
Katika mada za filamu, hadithi ya upendo bila shaka inapendwa zaidi kuliko mada zingine. Ni kweli kuna filamu zenye matukio ya kuvutia, vitendo vya ajabu na zingine za kutisha ambazo mimi sipendi. Lakini habari za upendo, nadhani, zinakuwa za kwanza. Kwa nini?
Sijui kama umeshachunguza filamu ya hadithi ya upendo; kuangalia mtiririko wa mada pamoja na wachezaji ili uelewe kwa nini tunavutwa sana nao? Kinachofaulisha filamu hizo ni kuona jinsi pendo linaloshinda licha ya mapingamizi mengi; wakati linashinda dhidi ya changamoto kubwa na majaribu mbali mbali.
Tunataka kuona jinsi pendo linavyostahimili na kushinda katika majaribu makubwa mno. Hii ndiyo inasababisha hadithi ya upendo kutuvuta sana. Ndiyo maana tunaiangalia. Ukweli huo unaoweza kutusaidia kuelewa zaidi mstari unaofuata:
1 Yohana 3:18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
Katika hali halisi ya maisha, upendo wetu unadhihirika kuwa wa kweli, wakati yale tunayoyatenda yanashinda mazingira yenye changamoto, wakati yanashinda majaribu makubwa mno … kwa niaba ya upendo.
Ni rahisi kumwambia mtu kwamba tunampenda. Ni jambo tofauti kabisa kuonyesha upendo kimatendo kwa kujitoa kwa ajili yake. Pendo lako liwe la kweli!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.