... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wakati Tunapenda Usalama Kupita Kiasi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 15:30-32 Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa? Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku. Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunyewe, maana kesho tutakufa.

Listen to the radio broadcast of

Wakati Tunapenda Usalama Kupita Kiasi


Download audio file

Tukiweka pembeni wanaopenda kuruka kwa parachuti na wanaopenda kupanda milima mirefu na wengine wanaochezea hatari, sisi wengine karibu wote tunajaribu kujiepusha na hatari.  Tunatamani usalama na kwenye karne yetu ya 21, dhana hiyo inaendana na anasa na starehe.

Tangu nilipovuka umri wa 65 hivi karibuni, nimeshangaa jinsi mtandaoni ninazidi kupokea ujumbe unaohusu swala la kustaafu – kunikadiria pesa zitakapohitajika, aina ya mahusiano ya kijamii ingenibidi kuanza kujenga na kadhalika.

Nimeshtuka kuona wanavyonivizia kwa kutumia mifumo yao ya teknolojia na ninaweza kukwambia kwamba aina hizo za ujumbe ni mtego kabisa.  Yaani, kuvutwa sana kujitenga katika usalama wako na starehe yako, hata kama wadunia wanashawishika sana navyo, sidhani kwamba ndiyo mapenzi ya Mungu kwetu kuishia miaka yetu inayobaki hapa duniani, sidhani.  Hayo ndiyo aliyoandika Mtume Paulo …

1 Wakorintho 15:30-32  Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa?  Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku.  Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani?  Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunyewe, maana kesho tutakufa.

Nakubali kwamba labda wewe na mimi hatujaitwa kuishi maisha ya hatari kama vile Mtume Paulo, lakini hata hivi, tukumbuke alivyosema mwandishi mmoja aitwaye John A Shedd aliyeishi karne ya 19, “Mashua bandarini ni salama kweli, lakini mashua haijaundwa kubaki bandarini tu.”

Usitafute sana starehe na anasa.  Yamkini Mungu ana mpango tofauti kabisa kwa ajili yako.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.