... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Watu Ambao Hawajakamilika

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 7:3-5 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Listen to the radio broadcast of

Watu Ambao Hawajakamilika


Download audio file

Hili ni swali linalosumbua. Ni yupi katika familia yako anayekusumbua sana?  Si nilikwambia kwamba ni swali gumu! Usikwepe!  Ni mume wako au mke wako?, ni mtoto mmojawapo, mzazi au mkwe?  Ni yupi anayekuchukiza zaidi?

Ni kweli, mtu anaweza kuchagua rafiki zake lakini hawezi kuchagua ndugu na jamaa. Kuna watu wenye utamaduni mzuri wa kukaa vizuri kifamilia kuliko wengine, lakini kadiri tunavyozidi kutajirika na kujitegemea wenyewe, ndivyo baadhi ya watu ndani ya familia wanazidi kutuchukiza.

Matokeo ni kwamba, mara nyingi kuna mpasuko ndani ya familia. Wazazi, watoto, ndugu, wakwe hawaongei miaka nenda-rudi. Tupokee maono hapo!  Hii haiendani na mapenzi ya Mungu hata kidogo! Sasa, mtu atafanyaje kuanza kuleta suluhisho?  Mtu anawezaje kuwa chombo mikononi mwa Mungu kuleta uponyaji ndani ya familia yake?  Yesu ndiye awezaye kutuonekania katika swala hilo :

Mathayo 7:3-5  Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?  Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe!  Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?  Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

Huoni kama muda umewadia wa kushuka na kukiri kwamba labda wewe umekuwa na sehemu katika matatizo ya familia yako?  Je! Si muda mwafaka kuwajibika wewe mwenyewe?

Angalia, Mungu anapenda familia yako. Anataka kuiletea uponyaji. Tuanze na wewe mwenyewe. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy