... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Weka Matendo Yako Nuruni

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 3:20,21 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Weka Matendo Yako Nuruni


Download audio file

Kama ningeweza kukuhoji uongee kwenye kipindi cha redio halafu nikikuomba uwaambie wasikilizaji kitu kile kimoja kilichomo maishani mwako ambacho kinakutia aibu, je!  Ungetaja nini?  Je!  Ungekuwa muwazi kiasi gani?

Binadamu wana siri zao, vitu ambavyo wasingependa kumwambia mtu ye yote, wakijua kwamba ni vibaya; kwamba havistahili kabisa; kwamba hakika, havimheshimu Mungu.

Je!  Mtu atawezaje kuviondoa?  Mtu anawezaje kuishi maisha ambayo hakuna hata kitu kimoja ambacho kikidhihirika, kingemwaibisha?

Yohana 3:20,21  Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.  Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.   

Ukifuata anachosema hapa Yesu, jibu ni kwamba mtu angeleta yote nuruni, kila wazo, kila tendo. 

Baada ya kufanya hivyo, mtu angeweza sasa kuweka yote nuruni, na kwa kweli, sisi sote tungependelea kuishi mahali hapo pazuri, si kweli?

Usidanganyike.  Hakuna kilichofichwa machoni pa Mungu.  Tena tujue kabisa kwamba siku ile tutakaposimama mbele zake katika hukumu, matendo yetu yote yatadhihirishwa.

Yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.