Ya Kale Yamepita
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Ebu fikiria ingekuwaje kama ungelazimishwa kubeba vitu vyako vyote unavyomiliki ndani ya begi mbili. Kadiri unavyonunua vitu vingine, ndivyo begi zile zinazidi kujaa na kukulemea. Kwa hiyo unanunua begi la mgongoni na ingine kuweka kwa bega moja. Hatimaye mizigo hiyo itakulemea sana hadi kusababisha ukose kuvuta pumzi vizuri, usiweze kupiga hatua mbeleni.
Kama ulipata nafasi kufuatana nami siku zilizopita, utafahamu kwamba tumesimulia mengi kuhusu kuachana na mambo yaliyopita. Labda unafikiri … Jamani! Kwa nini anarudia-rudia mada hii hivi?
Kuna sababu nairudia-rudia. Ni kwamba kuachana na mambo yaliyopita ni swala gumu sana kuliko yote mengine ambayo tungeyafanya. Kwa hiyo, leo siku ya kumalizia mwaka, ninaisisitiza tena kwa mara ya mwisho. Siyo lazima majukumu hayo magumu yakuangukie wewe peke yako. Huna haja ya kuhangaika kwa kujaribu kusahau maumivu na kujaribu kutibu majeraha yako. Kwa sababu hayo ni majukumu Yesu alikuja kukufanyia wakati alikufa na kufufuka kutoka wafu. Je! Uko tayari kupokea habari hiyo?
2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Ikiwa inakuwia vigumu kuvuta pumzi kwa sababu ya mizigo ya kale, kama umeshindwa hata kufikiri jinsi utakavyoweza kupata nguvu ya kupiga hatua na kuingia mwaka mpya, basi jua hili. Muda ule ule unaoweka tegemeo lake kwake Yesu, unakuwa mara moja kiumbe kipya. Ya kale yamepita. Yote yamekuwa mapya. Yesu anabadilisha kila kitu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.