Yesu Anaanza Kazi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mariko 1:14,15 Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Kuanzisha jambo jipya daima; ni kama kubahatisha. Mtu anaanza hatua ya kwanza akiwa na mashaka. Anataka aanze vizuri. Na Hataki kuwakwaza watu siku ya kwanza.
Zamani nilipokuwa mshauri katika mambo ya tekonolojia, kipindi naanza kusaidia mteja wangu mpya, yaani ilikuwa vigumu, nilikuwa najiuliza, hivi, Mazingira ya kampuni hii ni yapi? Nijihadhari vipi nisije kuwakwaza viongozi wangu?
Sasa, fikiria kwamba wewe ndio Mwana wa Mungu. Hadi sasa umefichwa salama salamini kijijini Nazareti; ndani ya kituo cha seremala ukitengeneza –viti, milango, labda jeneza. Lakini; hatimaye siku inawadia; inakubidi kuanzisha kazi ile Baba yako aliyokupeleka kuifanya duniani.
Sasa nikuulize, je! Yesu alifanyaje kuondokana na hali ya zamani na kuingia mambo mapya? Aliwezaje kutoka kwenye mazoea ya maisha yake ya awali na kuanzisha huduma ambayo hatimaye itamfikisha msalabani?
Mariko 1:14,15 Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Yohana Mbatizaji amewekwa gerezani – hivi punde atauawa, Mtu angefikiri kwamba; Yesu angesubiri kwanza; lakini hapana. Badala ya kutulia yeye anatangaza watu watubu dhambi zao; anasimama kinyume na tabia zao mbaya na anawaagiza waache uovu na kumrudia Mungu.
Yaani aliona uzito wa dhambi zao; na za kwetu pia kuwa kubwa mno, hadi pale alipokuwa tayari kutoa uhai wake kwa ajili yetu; ili atutoe katika hali hiyo.
Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.