... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Adui wa Msalaba

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:18,19 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.

Listen to the radio broadcast of

Adui wa Msalaba


Download audio file

Kuna jambo moja wazazi wanaliogopa sana, ni kwamba, wanaogopa mtoto wao asipotoshwe na rafiki wasiofaa na kufuata watu ambao si mifano mizuri kwa kuigwa.

Je! Unafikiri ni mara ngapi Mungu ameona mmoja wa watoto wake akipotoshwa kwa kuiga mfano wa watu wabaya? 

Kwahiyo, acha nikuulize, Ni akina nani wamekuwa mfano wakuigwa?  Ni akina nani wanaweza kukushawishi kwa urahisi na ukawaruhusu kuongoza mawazo yako hata mienendo yako?  Sasa hili ni swali nyeti:  Je!  Wanastahili kupokea heshima hiyo na kuaminiwa kwa kiwango hicho? 

Jana tuliongea umuhimu wa kuwa na watu wanaofaa kuwa mfano wa kuigwa maishani mwetu … ili kama wafuasi wa Yesu (ambao ni wanafunzi), tuweze kuwa wajenzi wake, tukijifunza huku tukiwa kazini. 

Lakini leo, tunaleta tahadhari kwa kuweka wasiofaa kuwa mifano yetu ya kuigwa.  Tumsikilize tena Mtume Paulo kuhusu hilo: 

Wafilipi 3:18,19  Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani. 

Kuna watu wanaojidai kuwa Wakristo, wakiigiza kana kwamba wao ni wafuasi waaminifu wa Kristo, lakini, mtu akichunguza matunda ya kazi zao, hata kama wanatumia lugha laini ya kushawishi, ni dhahiri kwamba si wa kweli! 

Usifungulie moyo wako watu wasiofaa.  Usipotoshwe na adui za msalaba! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy