... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ni Nani Aliye Mfano Kwako wa Kuigwa?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:17 Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Ni Nani Aliye Mfano Kwako wa Kuigwa?


Download audio file

Sidhani kuna mtu asiyetaka kuwa na maisha bora.  Sisemi tu habari ya kufaulu kupata vitu vya dunia, Sawa, hayo ni mazuri.  Lakini kuishi “maisha bora” hasa inatakiwa mtu abadilishwe ndani.

Ukiangalia nyuma wiki iliyopita, bila shaka ulikutana na visiki na vikwazo.  Yaani mambo yasiyokwenda kama ulivyotazamia.  Mambo yalisababisha mikwaruzano, mambo yaliyokuumiza – na kama ungepata nafasi ya kurudia wiki ile – bila shaka ungetenda vingenevyo ili yale yasitokee. 

Na kama tukisema kweli, kila mtu angekiri kwamba na yeye mwenyewe alichangia katika matukio yale yaliyoleta maumivu.  Ndiyo maana tukisema “maisha bora”, tunalenga swala ya sisi kujifunza zaidi, kubadilika na kushinda madhaifu na mapungufu yetu. 

Sasa, kuna sababu ya msingi kwanini useremala haufundishwi hasa darasani, bali, vijana wanaotamani kuwa seremala wanakuwa fundi stadi, kwa muda wa kutosha, wakijifunza ule ufundi huku wakiwa kazini. 

Wanaangalia mafundi wenye uzoefu mkubwa na kuwaiga hadi pale na wao wanafaulu kutengeneza vitu kama wao.  Kumbe, hiyo ndiyo kanuni katika sekta zote za maisha.  Hivi ndivyo Mtume Paulo alivyowaelezea rafiki zake huko Filipi: 

Wafilipi 3:17  Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi. 

Kwa miaka mingi sasa, nikisafiri pamoja na Yesu, mengi kati ya yale niliyojifunza yametokana na mimi kuwa “kazini” – yaani kuangalia wale wanaonizidi hekima, watu imara, kuangaia namna wanavyotembea na Yesu; nikiangalia mwitikio wao wakisongwa na mambo magumu; nikivutiwa na unyenyekevu wao na ucha Mungu wao. 

Watu wale tunawaita washauri wazuri, watu wa kuigwa.  Wana sehemu kubwa kwenye maisha yetu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.