... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Umwachie Yesu Akubadilishe

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 4:32 Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Umwachie Yesu Akubadilishe


Download audio file

Sijui ukoje, lakini mimi mwenyewe nakiri kwamba inaniwia vigumu mno kubadilisha tabia zangu mbaya zilizo sugu.  Kama ningesema ukweli, haiwezekani kabisa.

Sasa ni shida kabisa kwa sababu Neno la Mungu limetuagiza mara nyingi kuishi maisha ya maadili.  Kwa mfano: 

Waefeso 4:32  Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane … 

Hakuna awezaye kupinga agizo hilo.  Kama kweli unataka kuishi maisha mazuri, kama unataka kuangazia ulimwengu huu na nuru ya pendo la Mungu, kama unataka kuwa balozi mwaminifu wa Kristo, lazima uwe mtu mwenye fadhili, mwenye huruma ukipenda wanaokuzunguka.  Lazima uwasamehe, si mara moja tu, bali mara tena na tena kama vile Yesu alivyosema. 

Lakini ndugu, tuwe wakweli.  Wakati mtu ni mkorofi au anakuumiza hata kukusaliti au akikufokea tu, je!  Ni rahisi kwako kumhurumia na kuwa na fadhili kwake?  Je!  Ni rahisi kumsamehe mara tena? 

Tunachokihitaji ni kuwa na sababu ya kuwa wenye fadhili, wenye upendo na watu wanaoweza kusamehe muda ule ule tunapochokozwa.  Kinachohitajika zaidi ni uwezo.  Kwa hiyo acha nikupe mstari ule wote, nikiendelea kusoma pale mwisho ambapo uwezo unapodhihirika. 

Waefeso 4:32  Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.  

Kazi ile kubwa mno Mungu aliyetutendea, kwa kutusamehe kupitia mateso ya Yesu wakati alilipa deni la dhambi zetu pale msalabani, ni ajabu kabisa.  Yeye ndiye sababu tunaweza kusamehe.  Yeye ndiye uwezo.  Acha Yesu akubadilishe. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.