... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Unavyowaadhibu Wengine

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luke 6:37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.

Listen to the radio broadcast of

Unavyowaadhibu Wengine


Download audio file

Je!  Tuwe na mwitikio gani wakati watu wanatukosea?  Mtu atakabilianaje na wenye kumwudhi, watu wasiompenda, wanaomdhalilisha?  Nijibu, wewe binafsi unafanyaje?

Kikawaida, mwitikio wetu ni kujaribu kuwaadhibu.  Labda utafikiri kwamba nimejibu kwa haraka, lakini nivumilie kwanza.  Mfano, mtu anakukwaza, na unakwazika kweli.  Halafu, inategemeana na jinsi ulivyo, kama wewe ni mpole au mtu anayependa kukabiliana na mambo moja kwa moja.  Au utaumizwa vibaya na kujitenga au utakuja juu tayari kupigana.

Haijalishi unaitikiaje, kwenye kiini cha moyo wako utamhukumu na kwa njia moja au nyingine, utatafuta jinsi ya kumwadhibu.  Pengine utajitenga naye kabisa, au utaendelea kumwazia mabaya tu, au utaanza kumsengenya ukiwaambia watu wengine wasimwamini.

Yaani kuna aina nyingi za mwitikio mtu anazoweza kutumia, lakini zote zinahusu swala la kuadhibu, na kuwapa watu waliokuudhi yale wewe unaona wanayastahili kupata.  Isipokuwa tutamsikiliza Yesu kuhusu swala hilo:

Luke 6:37  Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.

Labda Andiko hilo unalijua vizuri sana lakini je!  Unalitumia kweli kweli kwa wale wanaokuumiza na kukuudhi?  Leo hii, Yesu bado anaongea nasi kwa nguvu kuhusu uhusiano wetu na watu wa namna hiyo.

Usiwahukumu, usiwalaumu bali uwasamehe.  Kwa sababu kuna matokeo kwetu, wewe na mimi, si katika mahusiano yetu na wao lakini pia katika jinsi Mungu atakavyotutendea na sisi.  Ujifunze kusamehe.

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.