... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Aliye Mwema Kuliko Wote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 6:35,36 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu. Basi iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Listen to the radio broadcast of

Aliye Mwema Kuliko Wote


Download audio file

Watu wanaweza wakatofautiana kwa jinsi walivyo na akili.  Pengine wewe una kipaji fulani wakati jirani yako anacho kipaji kikubwa tofauti kabisa.  Ndivyo ilivyokusudiwa iwe.

Sisi sote tunakosea kwa sababu 1) tunadhani watu wengine wote wanapaswa kuwa stadi katika yale ambayo tunayoweza kufanya sisi na 2) kama hawawezi tunawahesabu kuwa wapumbavu.

Je!  Unafikiri nimekuwa mkali?  La!  Hua inatokea mara nyingi tu.  Ni mara ngapi umejikuta unasema, “Sielewi kabisa kwa nini fulani hawezi kufanya hiki na kile.. ?”  Unachokisema kwa kweli ni kwamba, “Kwa nini asione mambo kama mimi ninavyoyaona?  Kwa nini hawezi kutimiza yale ambayo mimi ninayoweza kufanya kwa urahisi?”

Kwa sehemu ya kwanza ya maisha yangu, nilidharau kabisa watu ambao hawakuwa na akili kama mimi – nikiwafedhehesha na kusababisha wajione kuwa hawafai – huku mimi mwenyewe nikiwa kipofu nisione kwamba wao walikuwa na jambo bora.  Kumbe wao walikuwa na akili katika hisia zao.  Watu wema, wapole yaani walikuwa na sifa ambazo mimi nilizikosa kabisa.  Walikuwa na uwezo wa kuchukuliana na watu na kusitiri makosa ya wengine, hata maadui, wakiwatendea mema wale ambao waliokuwa wanawatendea visivyo.

Luka 6:35,36  Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.  Basi iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Hmmh.  Kumbe!  Inaonekana kwamba mwenye huruma yeye ndiye anayo akili kuliko wote wanaomzunguka.  Wapende adui zako.  

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.