... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Msijisumbue kwa Neno lo Lote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Mambo ya Nyakati 7:13,14 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, nakuomba, na kunitafuta uso, nakuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

Listen to the radio broadcast of

Msijisumbue kwa Neno lo Lote


Download audio file

Muda huu, yote yaliyotokea katika maisha yako hadi sasa, yameshapita kabisa.  Huwezi kuyarudia, lakini unaweza kuyaruhusu yaendelee kukusumbua.

Sijui kama umewahi kufikiri, lakini kujisumbua kwa yale yaliyopita ni kazi bure kabisa kuliko yote mtu angeyafanya.  Hakuna hata kitu kimoja katika yaliyopita ambacho unaweza kukibadilisha. 

Badala ya kufanya hivyo, wengi wanajisumbua wakifikiri juu ya mambo yajayo.  Sasa masumbuko hayo yote, yakihusu yaliyopita au yaliyopo sasa au yatakayokuja yanamlemaza mtu; yanamkwamisha asiweze kuyafanya yale ambayo yampasa ayatimize.  Yanamzuia asiishi uzima ule tele Yesu alikuja ampe.  Kwa hiyo, niulize, je!  Jibu linapatikanaje? 

2 Mambo yaNyakati 7:13,14 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, nakuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, nakuiponya nchi yao.

Shida, dhiki na taabu hua zinaweza kutoka kwa mkono wa Mungu, ni kweli.  Sasa, mwitikio wetu ungekuaje?  Kwanza nikutubu kama taabu imetokana na dhambi yetu.  Pili ni kuomba.

Kama vile mtu Fulani alivyosema, kujisumbua ni masimulizi mtu anafanya na yeye mwenyewe kuhusu mambo ambayo hawezi kuyabadilisha.  Kuomba ni masimulizi mtu anafanya na Mungu kuhusu mambo ambayo yeye Mungu anayoweza kubadilisha. 

Jinyenyekeshe na uombe.  Halafu kadiri inavyokuhusu, acha njia zako mbaya.  Mungu atakusikia.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.