... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ondokana na Uovu Wako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 1:21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.

Listen to the radio broadcast of

Ondokana na Uovu Wako


Download audio file

Inaonekana kwamba kuna njia moja tu ya kujiepusha kabisa na uovu unaotawala ulimwengu huu na kuenena kila sehemu ya maisha.  Ni kujitenga kabisa na kuishi peke yako.  Hmm.  Au sio?

Hivi karibuni nilipokea barua pepe kutoka kwa mtu mmoja aliyeamini Kristo kwa kupitia vipindi vyetu vya NENO SAFI NA LENYE AFYA.  Lakini kwa sababu ya sehemu anamoishi, lazima aendelee kubaki mwamini wa siri kwa sababu ya kuogopa kuteswa vibaya.  Bado anaishi katika nyumba ya wazazi wake, ambamwo kuna sanamu ndani ya kile chumba.

Haijalishi unaishi wapi au katika mazingira gani.  Haijalishi umezama katika utamaduni gani, maisha ndivyo ilivyo.  Uovu unaonekana kote kote.  Sasa Mungu anatuonya kupitia Yakobo, ndugu yake Yesu, akifahamu hali zetu kwa kutwambia hivi:  

Yakobo 1:21  Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.

Wewe na mimi, hatuwezi kuondoa uovu wote uliopo duniani.  Pia, bila kujitenga kabisa, hatuna budi kukutana nao.  Lakini kitu Mungu anachokisisitiza katika mstari huu ni kitu kingine.

Anatwambia tuweke mbali uovu wote ndani ya maisha yetuubaya wote aina yote tunaoufanya sisi halafu tupokee kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zetu. 

Rafiki yangu, unaweza kuwa unaishi ndani ya nyumba iliyojaa sanamu na kuamua kutokuziabudu.  Unaweza kuzungukwa na uovu na kuamua kutokushiriki nao.

Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.