... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tazamia Kuona Mambo Makuu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 126:1-6 BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto. Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu. BWANA alitutendea mambo makuu, tulikuwa tukifurahi. Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa, kama vijito vya Kusini. Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, aichukuapo miganda yake.

Listen to the radio broadcast of

Tazamia Kuona Mambo Makuu

Download audio file

Najiuliza mara kwa mara kwamba wakati tunaomba, mara ingine tunamwendea Mungu na matazamio yaliyo hasi.  Je!  Ananisikia kweli?  Je!  Ananijali?  Je!  Yupo kweli kweli?  Matazamio hasi kabisa.

Usinielewe vibaya.  Mimi si mmoja wao wa wale wanaosema, “Litaje, lidai” au “Tamka, ushike” wala.  Tunajua kwamba katika yote Mungu ndiye mwenye enzi; mapenzi yake yatatimizwa.  Lakini hata hivi, Maandiko yamejaa mifano ya maombi mengi yenye matazamio makuu.  Hili ni ombi mojawapo:

Zaburi 126:1-6  BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto.  Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, na ulimi wetu kelele za furaha.  Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu.  BWANA alitutendea mambo makuu, tulikuwa tukifurahi.  Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa, kama vijito vya Kusini.  Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.  Ingawa mtu anakwenda zake akilia, azichukuapo mbegu za kupanda.  Hakika atarudi kwa kelele za furaha, aichukuapo miganda yake.

Sisemi kwamba Mungu lazima acheze kufuatana na pigo la ngoma yetu wala lazima atupe kila tamanio tulilo nalo, hapana.  Isingeeleweka.  Lakini Zaburi hii tutoka kusoma ina matazamio makuu kwa kweli.  Kuna neno moja aliloandika mchungaji wa Afrika wa Kusini kwenye karne ya 19 aitwaye Andrew Murray ambalo linalovuma katika mada hii:

Kila mara kabla hujafanya maombezi, tulia kwanza ukamwabudu Mungu katika utukufu wake.  Tafakari juu ya yale awezaye kutenda na jinsi anavyopendezwa sana kuyasikia maombi ya watu wake waliokombolewa.  Tafakari nafasi uliyo nayo na fursa yako ndani ya Kristo halafu uyatazamie mambo yaliyo makuu.

Watakayokwenda zao wakilia, watarudi kwa kelele za furaha.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.