... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wasamehe Waliotubu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 17:1-4 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. Jilindeni; kama ndugu yako akikosa mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

Listen to the radio broadcast of

Wasamehe Waliotubu


Download audio file

Uwezo wetu wa kusamehe, wewe na mimi, ni kama msuli unaohitaji kuzoezwa ili uzidi kupata nguvu.  Kumbe!  Tunaishi katika dunia ambayo kuna nafasi kubwa ya kuzoeza!

Siku hizi chache tumesimulia habari ya dhambi kufuatana na mafundisho ya Yesu mwenyewe.  Kwanza, alisisitiza kwamba kujaribiwa ni jambo la kawaida kwa kila mtu.  Pili, tukishindwa na jaribu fulani, mara nyingi tunavuta wengine kutenda visivyo, jambo ambalo Yesu analichukulia kwa uzito kabisa. 

Luka 17:1-3a  Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!  Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.  Jilindeni. 

Hoja yake inalofuata na yenyewe ni muhimu sana. 

Luka 17:1-3b,4   Kama ndugu yako akikosa mwonye; akitubu msamehe.  Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe. 

Yesu alikufa msalabani pale ili tuweze kusamehewa, ili minyororo ya dhambi ivunjwe na matokeo yake yabatilishwe.  Ndiyo maana swala la msamaha ni muhimu sana machoni pa Mungu.  Na hata kwetu, linapaswa kuwa muhimu pia wakati mtu anatukosa.  Je!  Unataka kuvunja pingu za mnyororo ule?  Je!  Unataka kusitisha matokeo ya dhambi yao isiendelee? 

Wakati mtu anakukosa, lazima umwonye.  Lakini akitubu (hata kama amerudia kosa mara tena) … msikilize vizuri alivyosema Yesu, … lazima umsamehe.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.