... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiwe Mwenye Kuleta Kikwazo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 17:1-3a Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. Jilindeni.

Listen to the radio broadcast of

Usiwe Mwenye Kuleta Kikwazo


Download audio file

Kuna uongo Shetani anapenda kueneza kwamba “dhambi ndogo” haina shida.  Endelea, hakuna atakayekuona!  Ni dhambi ndogo tu.  Ni kama si dhambi nyenyewe.

Huu ni uongo anaopenyezewa mara tena na tena masikioni mwa kila mtu anayempenda Yesu.  Yaani ni uongo uliotengenezwa kwa ustadi kwa sababu inaeleweka masikioni mwa mtu anayetaka kukubali kishawishi anachoona kuwa kidogo tu.  Hakuna atakayemwona.  Hakiwezi kumdhuru mtu. 

Lakini dhambi haiwezi kufichwa, pia dhambi daima ina matokeo yake.  Tokeo moja ni kwamba dhambi ile unayeiona kuwa ndogo sana kumbe inaweza kuwashawishi watu wengine kukufuata katika uovu. 

Mfano, ukinung’unika masikioni mwa familia yako, ni kama unawafundisha na wao wanung’unike.  Ukimfokea mtu, inawezekana Mkristo mchanga anaweza kuanza kuiga tabia yako mbaya.  Sasa hii ni jambo ambalo Yesu analichukua kwa uzito kabisa. 

Luka 17:1-3a  Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!  Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shindoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.  Jilindeni. 

Wakati tunawakosesha watu wengine na kusababisha watende dhambi, tunakuwa chombo anachokitumia Shetani, ndiye Ibilisi ambaye anataka kupotosha watu wa Mungu.  Ndiyo maana Yesu anaichukulia kwa uzito kabisa.  Siyo mchezo hata kidogo. 

Usiwe mtu yule ambaye anakosesha wengine kwa kuleta kikwazo.  Acha kabisa!  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.