... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tafuta Hekima Mapema

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 3:13-18 Heri mtu yule aonaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Njia zake ni njia za kupendeza sana, na mapito yake yote ni amani. Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; ana heri kila mtu ashikamanaye naye.

Listen to the radio broadcast of

Tafuta Hekima Mapema

Download audio file

Je!  Unakumbuka wakati ulikuwa bado kijana na jinsi ulivyopumbazika mara kwa mara?  Mimi ninakumbuka vizuri sana mambo ya upumbavu niliyoyafanya nikiwa kijana

Balaa mojawapo maishani ni kwamba mtu anazeeka mapema lakini anapata hekima iliyochelewa.  Ni kweli kabisa!  Hekima, mtu akiipata, mara nyingi hua inatokana na kuishi miaka mingi katika pirika za kusuguana katika maisha haya.

Lakini je!  Ingekuaje kama mtu angeanza kupata hekima mapema?  Ingekuaje kama mtu angewawahi wenzake kuhekimishwa?  Maisha ya mtu Yangeborekaje kama angekuwa na hekima wakati yeye bado ni kijana?

Sikiliza jinsi mzee Mfalme Sulemani alivyowaambia vijana wake kuhusu mada hii:

Mithali 3:13-18  Heri mtu yule aonaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu.  Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.  Yeye ana thamani kuliko marijani, wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.  Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.  Njia zake ni njia za kupendeza sana, na mapito yake yote ni amani.  Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; ana heri kila mtu ashikamanaye naye.

Kwa kweli, hekima ya Mungu inaweza kutuletea mabadiliko makubwa mazuri maishani mwetu.  Kwa kweli, baraka zinazotokana na hekima yake hazipimiki.  Kwa hiyo jaribu kujibarikia, tafuta hekima mapema iwezekanavyo kwa sababu hekima ni baraka kwa wao wanaoishika sana.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.