... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Fuata Barabara Iliyo Juu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:18-20 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani. Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Fuata Barabara Iliyo Juu


Download audio file

Dunia imejaa mambo mengi ya kuzubaisha.  Mengine ni mema kabisa, aina ya burudani.  Lakini kidogo kidogo, burudani ikiongezeka kupita kiasi, hatimaye inaweza kumpelekea mtu kutereza kabisa na kuporomoka kwenda mbali na Mungu.

Ninaomba Mungu akubariki na kukupa riziki, sehemu ya kulaza kichwa chako na kukupa mavazi na ndugu na marafiki mnaopendana.  Zaidi ya hayo, ni jambo jema kuwa na burudani kama vile kuangalia filamu nzuri au kuwa shabiki ukisapoti timu unayoipenda zaidi.  Jambo lingine zuri ni kuchukua muda wa likizo na kutalii kidogo ikiwezekana. 

Hayo yote hayana mabaya isipokuwa … yanaanza kuwa kipaumbele kwetu na kuchukua nafasi ya kwanza katika maisha yetu.  Pale ambapo tunaanza kutamani burudani na starehe hizo zaidi na zaidi, ndipo zinapoweza kutupeleka mbali na Mungu ki-mawazo, katika masimulizi yetu, zikiongoza matendo yetu na matazamio tuliyo nayo.  Tukitawaliwa na mambo hayo, hatimaye tunageuka kuwa adui wa msalaba wa Kristo.  Sikiliza: 

Wafilipi 3:18-20  Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.  Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo. 

Je!  Wewe uaenendaje katika safari ya maisha yako?  Kama adui wa msalaba wa Kristo, kama mtu ambaye haridhiki, mtu ambaye hana furaha, mtu aliyechagua barabara inayoenda chini ikielekea uharibifu? 

Lakini wewe na mimi tu raia wa mbinguni.  Tunamsubiri Yesu arudi.  Rafiki yangu, katika safari yako, katika mwenendo wako maishani, Mungu amekuita upitie barabara iliyo juu.  Usiwe adui wa msalaba.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.