... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wewe niwa Kabila Gani?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wagalatia2:20 nimesulibiwa pamoja na kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilionao sasa katika mwili, ninao katika imani ya mwana wamungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi ya ke kwa ajili yangu.

Listen to the radio broadcast of

Wewe niwa Kabila Gani?


Download audio file

Tangu enzi za kale, binadamu wamejigawa katika makabila – kufuatana na jiografia, utamaduni, rangi ya ngozi, siasa na hata ushabiki wa timu ambayo tunapenda kusapoti.

Kanuni moja muhimu katika msimamo wa ukabila, ni kuhakikisha kwamba kabila lile lingine lisiweze kutuonea; kwamba wasinyang’anye eneo letu au wasitudharau.  Kwa vyovyoote, nina haki kuendelea kuwa kama nilivyo.  Nina haki kutambulika na kuwa mmoja wa kabila langu na kupata haki zangu zote. 

Kwa hiyo, acha nikuulize, je!  Wewe ni wa kabila gani?  Swali la pili, je!  Kuwa mwanachama wakabila yako inamgongano gani juu ya uhusiano wako na Mungu?  Kuna mchungaji Mmarekani akiwa pia mwandishi aitwaye Dale Partridge aliandika hivi: 

“Wewe uwe kama ulivyo” ni mwitikio bandia wa Shetani kupinga anavyosema Mungu, “Uwe mtakatifu kama nilivyo mtakatifu.”  Mimi sitaki kuwa mimi, bali niko sambamba na Mtume Paulo aliyesema … 

Wagalatia2:20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala simimi tena, bali Kristo yuhai ndani yangu; na uhai nilionao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Alichotaka kusema huyo ndugu Partrige, na mimi ninakubaliana naye, ni kwamba siku hizi kuna watu wengi sana wanajiita Wakristo lakini wanaruhusu utambulisho wao katika dunia hii kushinda utambulisho wao ndani ya Kristo. 

Mimi niwa chama hiki cha siasa.  Mimi ninatetea uhuru huu.  Hii ndiyo jinsia yangu.  Ndivyo nilivyotu.  Je!  Umewahi kusikia watu wanatetea hivyo?  Lakini kama unamwamini Yesu, basi ujue hili:  Alikuja ili akuokoe na jinsi ulivyokuwa. 

Umesulibiwa pamojana Kristo; lakini uhai; wala si wewe tena, bali Kristo yu hai ndani yako.

Usikubali ukabila ukunyanyase na kufanya usahau jinsi ulivyo ndani ya Kristo.

Hili ndilo Neno la Mungu safina lenye afya kwaajili yako leo.