... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kushindwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 149:4 Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake, huwapamba wenye upole kwa wokovu.

Listen to the radio broadcast of

Kushindwa


Download audio file

Jumamosi kati ya Ijumaa Kuu na Jumapili ya Pasaka.  Siku hiyo tunaifanyaje?  Ni kama hakuna kilichotokea kati ya matokeo yaliyotisha ya Ijumaa Kuu na mambo ya ajabu mno yaliyotokea siku ya Jumapili ya Ufufuo.

Je!  Unafikiri wanafunzi walikuwa wanafanya nini siku ile ya Jumamosi kabla ya Pasaka?  Je!  Walikuwa wanatulia tu wakifurahia mapumziko ya Sabato?  Je!  Walikuwa wanasubiri Jumapili ya Ufufuo ili waweze kusherehekea?  Sidhani!

Pengine walikumbuka utabiri wake Yesu kwamba angefufuka kutoka wafu.  Lakini mimi nadhani walikuwa bado wamechanganikiwa kwa sababu ya matukio ya Ijumaa.  Pia walikuwa bado wanahofia usalama wao, kwa hiyo bila shaka, walikuwa wanajificha.

Miaka michache kabla ya hapo, Yesu alikuwa ameshawaambia kwamba yeye ni mnyenyekevu wa moyo.  Baada ya miaka kadhaa, Mtume Paulo aliweza kuliandikia kanisa la Filipi, kwamba Yesu alijinyenyekesha hadi kifo, kifo cha msalaba.

Ukifikiria, Mwana wa Mungu, Muumba wa mbingu na nchi, kukubali kusulibiwa ili atuokoe wewe na mimi, bila shaka ni tendo kubwa la unyenyekevu lililowahi kutokea katika enzi zote.

Wimbo wa zamani wa Israeli, Zaburi 149, unamtukuza Mungu kwa ajili ya wema wake kwa watu wake.

Zaburi 149:4  Kwa kuwa BWANA  awaridhia watu wake, huwapamba wenye upole kwa wokovu.

Mungu ni mwenye msimamo, thabiti daima, la sivyo, yeye asingalikuwa Mungu.  Anapenda sana kupa thawabu wanyenyekevu.  Na siku ya leo, siku ambayo hatusomi tukio lo lote kati ya Ijumaa Kuu na Jumapili wa Ufufuo, ni kama andiko hilo linadokeza tukio ambalo lilikaribia kutokea.

Kushindwa vibaya kuliko vyote katika historia ya wanadamu, kumbe!  Kulitaka sasa kugeuka kuwa ushindi mkubwa kuliko vyote katika enzi zote kwa sababu Mungu anawaridhia wapole na kuwapamba wokovu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.