... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usione Haya Kwa Sababu Umefeli

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 1:8 Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Usione Haya Kwa Sababu Umefeli


Download audio file

Hatupendi kukiri kwamba tumeshindwa kwa sababu kufeli katika mtazamo wa kisasa wa mafaniko ni balaa.

Bila shaka umewahi kufeli katika maisha yako – na kwa mambo madogo ambayo umefaulu kuyaficha wengine wasijue, na kwa mambo makubwa ambayo yalikuwa dhahiiri tena yalisababisha watu wakudharau. 

Kawaida, watu wanajaribu kwa njia zote kuficha jinsi walivyoshindwa.  Lakini tukitafakari kwanza, nadhani kila mmoja wetu angekiri kwa yule ambaye amekusudia kutumia vipawa na vipaji alivyo navyo kwa ajili ya utukufu wa Mungu, kuna wakati atakosea; kuna kuna wakati atashindwa na jambo fulani katika safari yake.

Sasa mtu akishindwa atafanyaje?  Je!  Akifeli anawezaje kukabiliana na kufeli kwake?  Tumsikilize tena Mtume Paulo akiongea na mwanafunzi wake Timotheo: 

2 Timotheo 1:8  Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu. 

Yesu alionekana kana kwamba alifeli kabisa kuliko wote katika historia ya wanadamu wakati alitundikwa pale msalabani.  “Usimwonee haya mtu huyo.”  Hata Mtume Paulo pia, jamani!  Alionekana kwamba alifeli kabisa akifungwa gerezani.  “Usinionee haya mimi.”  Halafu tukimgeukia Timotheo (na hata sisi wenyewe) tunaambiwa, “Vumilia mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili.”  (Kumbuka kwamba kwa kizazi chetu, mtu akipata mateso ni kama amefeli). 

Sasa mtu atafanyaje akifeli?  Usiwe na haya, kwa sababu Mungu atakupa nguvu kupitia hali hiyo ya kushindwa.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.