... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mtumaini Bwana kwa Moyo Wako Wote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

MIthali 3:5,6 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.

Listen to the radio broadcast of

Mtumaini Bwana kwa Moyo Wako Wote


Download audio file

Katika safari yako, ukiwa steringi tuseme, sijui kama umeishaona jinsi steringi inaanza kucheza-cheza baada ya gari lako kupitia mashimo na kukata makona makali na mengi.  Ndivyo imani ya mtu inaweza kuyumbishwa-yumbishwa.

Kama umeshapitia haya, basi, acha nikutie moyo.  Si wewe tu peke yako.  Hua inatutokea sisi sote.  Na mimi pia nimeshayaona.  Na kuna sababu hua inatokea.  Ni kwa sababu Mungu anataka kutufanya tuwe watu wazima, kwa hiyo anaruhusu tupambane na mazingira ambayo yanapima imani yetu; mazingira ambayo yanasababisha tuzoeze imani yetu ili izidi kuwa na nguvu. 

Mashimo yale, makona makali yote yasiyotazamiwa, kumbe!  Yanawekwa kwa makusudi njiani tunapopita ili tuzidi kumtegemea Mungu.  Kwa hiyo, rafiki yangu; kama umekata shauri la kumfuata Yesu, halafu unajikuta kama ndege aliyekatwa mabawa yake halafu unashuka chini kwa kasi … basi ujue kwamba ndivyo Mungu alikupangia. 

Mahali pale, katika hali iyo hiyo, anataka wewe (na mimi pia) tufanye kama ilivyoandikwa: 

MIthali 3:5,6  Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako. 

Ndege akishakatwa mabawa, hana jinsi, hata akifanyeje.  Na wewe, kama mambo yanakuzidi kabisa usiyaelewe hata kidogo, kuzitegemea akili zako ni kazi bure.  Sasa mtu angefanyaje? 

Umtegemee Mungu kwa njia zako zote, umheshimu kwa kila wazo, kwa kila neno na kila tendo na kuendelea kutenda mema hata kama bado una hofu.  Ndipo utaona ahadi ya Mungu inatimia.  Atanyosha kila kitu. 

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.