Ahera Yako Inakungoja
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:21 Atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Sijui kama utaniwia radhi kama nitaonekana kuwa mtu anayehukumu leo? Mimi naona kama sisi tunaojiita kwa jina la Kristo – yaani Wakristo – sidhani kama tunatumia muda wa kutosha kufurahia Habari Njema za Yesu na kuionea fahari.
ninamkumbuka mwalimu mmoja niliyekuwa naye wakati ninasoma kwenye chuo cha Biblia – jina lake ni Ian Pennicook – wakati ananifundisha kuhusu Msalaba wa Kristo, alianza kutoa machozi kwa sababu ya yale Yesu waliyomtendea.
nakumbuka siku moja akisongwa na machozi, alisema hivi, “Samahani. Mimi siwezi kuongea hivi hivi kuhusu msalaba. Lazima tuuonee fahari kabisa.” Uzito wa maneno yake bado uko ndani yangu kupitia milima na mabonde na uchovu wa maisha haya, bado utukufu na fahari ya Msalaba wa Kristo vimejaa moyoni mwangu.
Tena isitoshe, utukufu huo ulitokana na yale Yesu aliyokutendea na kunitendea mimi na kumtendea mtu yeyote ambaye angemwamini na kutubu dhambi zake, utukufu huo utaendelea kufurika ndani yetu milele na milele.
Wafilipi 3:21 Atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Yale yote Kristo aliyoyashindia pale Msalabani yatakuwa mali yetu kupitia uwezo wake milele daima.
Sijui uko wapi – yamkini leo ni siku ya kawaida, au labda umechangamka, au pengine umekatishwa tamaa – lakini haijalishi hali uliyo nayo leo, kumbuka Msalaba. Ona fahari juu yake, Halafu ujue kwamba fahari yake pamoja na utukufu wake vitakuwa urithi wako milele na milele.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.